1 WAKORINTHO 15:45-49
Ndivyo ilivyoandikwa, mtu wa kwanza, adamu, akawa
nafsi iliyo hai; adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. lakini
hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.
mtu wa kwanza atoka kwa nchi, ni wa udongo. mtu wa pili atoka mbinguni.
kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye
wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. na kama tulivyoichukua
sura yake yule wa udongo kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa
mbinguni.
No comments:
Post a Comment